Waziri
wa habari , sanaa na michezo mh Harrison mwakyembe amependekeza kuwa
wanaoshiriki mashindano ya urembo wa ma-miss waajiriwe katika shirika la
ndege la taifa kwa sababu wana vigezo vya kutosha.
Mh
Harrison Mwakyembe aliyasema hyo katika uzinduzi wa mashindano hayo kwa
mwaka 2018 yatakayofanyika chini ya kampuni ya The Look baada ya ile ya
Lino kuachia ngazi hiyo.
Mh
Waziri amesema kuwa washiriki wengi wa mashindano hayo wanakuwa na
uwezo na sifa nyingi za kuwa katka cabin crew ila tu kabla ya kuajiriwa
wanapaswa kupelekwa kozi fupi ya miezi mitatu katika chuo cha anga kabla
ya kuanza kazi na hii itapunguza tatizo la ajira kwa warembo hao.
Hii
pia inaweza kusaidia baadhi ya wasichana kwa sababu kuna warembo
wamekuwa wakishiriki mashindano hayo na baadae dira zao za maisha
kupotea na kujikuta wakiishi maisha magumu sana.


0 comments:
Chapisha Maoni