Dansa
kutoka WCB ambaye ni mchezo shoo wa staa wa Bongo fleva Diamond
Platnumz, Zungu amekumbwa na skendo ya kuwa mmoja kati ya wanaume
waliotelekeza watoto wao Dar.
Siku
ya jumatatu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliwakusanya
wanawake wote ambao wametelekezwa na wanaume ambao wamezaa nao ambapo
hawawahudumii watoto wao.
Mmoja
kati ya Wanawake waliojitokeza ni mwanamke ambaye alijitambilisha kama
mzazi mwenza wa Dansa wa Diamond anayejulikana kama Zungu ambapo alidai
alimtelekeza yeye pamoja na mtoto wake baada ta kuachana ambapo amekuwa
hataki kumtunza mtoto wake.
Baada
ya tuhuma hizo Zungu alitafutwa na Timamu Tv ambapo amefunguka na
kusema yule mwanamke ana matatizo ya akili pia ni mkorofi na amedai kuwa
hajawahi kumkataa mtoto wake na amesema yupo tayari hata leo kwenda kwa
Makonda na kujielezea na kama ikitokea anatakiwa amchukue mtoto wake
amesema yupo tayari kumlea mwanaye mwenyewe.
0 comments:
Chapisha Maoni