Serikali
imesemachanjo ya saratani ya shingo ya uzazi haizuii magonjwa ya
kuambukiza yanayotokana na ngono zembe kama vile Ukimwi, kaswende na
kisonono.
Kauli
hiyo imetolewa jana bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile wakati akijibu swali la
nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Faharia Khamis Shomari.
Mbunge
huyo alitaka kujua iwapo chanjo hiyo ya saratani inazuia magonjwa
yatokanayo na ngono zembe kwa sababu vijana wanaanza kujihusisha na
vitendo katika umri mdogo.
Akijibu
swali hilo Dk. Ndungulile amesema serikali imezindua chanjo dhidi ya
saratani ya shingo ya uzazi kwa kuanza na na mabinti wenye umri wa
miaka 14.
“Baada
ya hapo watafuata wa miaka tisa hadi 13. Aidha tafiti zimeonesha kuwa
vijana wadogo wanajihusisha na ngono zembe hivyo niwaonye mabinti kuwa
chanjo ya saratani ya shingo ya uzazi haitawakinga dhidi ya magonjwa
mengine ya kuambukiza kama ukimwi, kaswende na kisonono,” alisema.
Aidha,
ametoa rai kwa wabunge na wananchi wote kuwa chanjo hiyo ni salama na
lengo la serikali ni kuhakikisha Taifa linaondokana na tatizo la
saratani ya shingo ya kizazi.
0 comments:
Chapisha Maoni