Mmoja
wa wahariri waandamizi wa gazeti la The Guardian, Finnigan Simbeye
ameokotwa eneo la Bunju wilayani Kinondoni akiwa hajitambui.
Taarifa
zilizosambaa leo Jumapili Aprili 8, 2018 zinazoonyesha kitambulisho
chake cha kazi cha kampuni ya The Guardian Limited zinaeleza Simbeye
aliokotwa akiwa kwenye hali mbaya.
Hata hivyo, kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni, Murilo Jumanne amesema hana taarifa za tukio la kuokotwa Simbeye.
Rose
Mirondo, ambaye ni mkewe Simbeye amesema mumewe aliondoka nyumbani jana
Jumamosi Aprili 7, 2018 akiwa na gari lakini hakurudi hadi alipopata
taarifa za kuokotwa kwake leo.
Amesema alipokwenda eneo la tukio Bunju hakuliona gari la mumewe.
Rose amesema watu aliowakuta eneo la tukio wamemweleza kwamba Simbeye alichukuliwa na polisi kupelekwa hospitali.
Amesema bado hana taarifa ya hospitali gani amepelekwa na kwamba, anakwenda Kituo cha Polisi Bunju kupata taarifa zaidi.



0 comments:
Chapisha Maoni