Binti
wa miaka 20 ambaye jina lake halikutajwa anashikiliwa na Jeshi la
Polisi Temeke jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kumuua mtoto wa miaka
miwili, ambaye ametajwa ni mdogo wake na kisha kumficha uvunguni mwa
kitanda huko nyumbani kwao Kigamboni jijini Dar es salaam.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Temeke Emmanuel Lukula amesema
tukio hilo limetokea Jumatatu ya April 23, ambapo binti huyo alimchoma
na kitu chenye ncha kali sehemu ya kitovu mtoto huyo na kumlaza kifudi
fudi, kisha kutokomea kwa mpenzi wake.
“Ni
kweli tukio hilo limetokea,aliyefanya hilo tukio ni binti wa miaka 20
ambaye ni ndugu wa mama wa marehemu, alimchoma huyo mtoto na kumlaza
kifudifudi uvunguni kisha akaondoka kwa mwanaume anayedaiwa kuwa na
uhusiano wa kimapenzi, na baada ya mama wa mtoto kurudi kazini hakumkuta
nyumbani”, amesema Kamanda Lukula.
Kamanda
Lukula ameendelea kueleza kwamba baada ya hapo mama alitoa taarifa
polisi, na baada ya uchunguzi walimkamata binti huyo na kuonyesha mahali
alipomficha mtoto huyo, na mpaka sasa anashikiliwa jeshi la polisi ili
hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
0 comments:
Chapisha Maoni