Chama
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimelitaka Jeshi la Polisi nchini
kutoa taarifa rasmi juu ya matukio ya kuwakamata na kuwapekua viongozi
wa kisiasa katika ngazi mbalimbali nyakati za usiku bila ya kuwepo na
sababu zozote zenye misingi ya kisheria.
Hayo
yameelezwa na taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na
Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene leo Aprili 25, 2018 na
kusema jeshi hilo limeendelea kuwashikilia kinyume cha sheria kwa
kuwanyima dhamana na kutowafikisha mahakamani
Aidha,
Makene amesema baadhi ya maeneo ambayo hadi sasa viongozi wa CHADEMA
wamekumbana na manyanyaso na ukiukwaji huo mkubwa wa haki za binadamu na
sheria za nchi unaofanywa na polisi ni Dar es Salaam, Geita, Pwani,
Njombe, Iringa, Arusha, Morogoro na Tanga.
"Tunapinga
na kulaani vikali vitendo hivyo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na
sheria za nchi yetu na tunasisitiza kuwa havikubaliki katika jamii
yeyote inayozingatia kuwa haki ni msingi muhimu wa amani na utulivu wa
kweli.Tunatumia nafasi hii kulikumbusha Jeshi la Polisi nchini kuwa lina
wajibu wa kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Katiba, Sheria za
Nchi na weledi unaokubalika", amesema Makene.
Kwa
upande mwingine, Makene amesema chama chake kimetoa maagizo kwa
wanasheria wake kupitia Kurugenzi ya Katiba na Sheria, kufuatilia suala
hilo kwa ukaribu na kuchukua hatua za haraka za kisheria.
0 comments:
Chapisha Maoni