test

Alhamisi, 29 Machi 2018

Mimi Mars: Sitaki Kuolewa na Mwanaume Mpare


Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Papara’ Mimi Mars ambaye pia ni mdogo wa staa wa Bongo fleva Vanessa Mdee, amefunguka na kuweka wazi kuwa hataki Kuolewa na mwanaume kabila la Wapare.

Mimi Mars amesema kuwa hategemei na wala hataki kuolewa na mwanaume kutoka katika kabila la wapare kwa sababu yeye mwenyewe ni mpare na kuna baadhi ya tabia za wapare anazijua na hazimpendezi.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Mimi Mars pia ametaja Makabila mengine kama wachaga ambayo nayo amekiri hatorudia Tena kuwa nao:
"Kutokana na mimi mwenye kuwa ni Mpare kwa hiyo tabia za wanaume wa kipare ninazifahamu vizuri halafu wanasema mafahari wawili hawezi kukaa zizi moja, hivyo najua tutashindwana tu kwasababu wote tunajisikia, wabahili 'so' tukikaa wawili 'type' hiyo mambo yatakuwa magumu", amesema Mimi Mars.

Pamoja na hayo, Mimi ameendelea kwa kusema; "inanibidi nitafute kabila ambalo tofauti na mimi ndio maana sitoweza kuwa kabila hilo ila sio kwa ubaya ila mimi mwenyewe tu nimesema sitoweza.

Lakini pia Mimi Mars ameweka wazi kuwa kwa sasa hana mpenzi  na yupo single:

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni