Kamanda
wa Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema
wamejipanga vizuri katika kuimarisha hali ya usalama nchini katika
sikukuu hii ya Pasaka na kudai atakayethubutu kufanya vitendo vya
kiharifu atachukuliwa hatua kali.
Kamanda
Mambosasa ameeleza hayo leo (Machi 30, 2018) wakati alipokuwa
anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kusema
kulingana na uzoefu waliokuwa nao wamejipanga kuimarisha usalama kwa
hali ya juu ili wananchi waweze kusherehekea kwa amani na utulivu.
"Jeshi
la Polisi litahakikisha wananchi wa Dsm wanasherehekea sikukuu hii kwa
amani na utulivu na kwa kuwa uzoefu unaonesha kwamba mara nyingi katika
sherehe kama hizi watu wenye nia ovu wanajiandaa kufanya vitendo vya
kiharifu ikiwa na pamoja na kufanya ujambazi ili kujipatia vipato
kwaajili ya kusherehekea sikukuu", amesema Mambosasa.
Pamoja
na hayo, Mambosasa ameendelea kwa kusema "baada ya kulijua hilo Jeshi
la Polisi tumejipanga vizuri, kwamba hakuna mtu yeyote atakayeweza
kupata fursa ya kufanya lolote katika uvunjifu wa sheria, tumeimarisha
doria lakini tunaendelea na misako maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam
katika mikoa yote mitatu na wilaya zote za kipolisi 11".
Kwa
upande mwingine, Kamanda Mambosasa amesema hayo yote yanafanyika kwa
lengo la kuimarisha hali ya usalama katika siku kama hizi za sikukuuu.
0 comments:
Chapisha Maoni