Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeutaka uongozi wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam kurekebisha mkataba kati yake na kampuni ya Mlimani
Holding Ltd kutokana na upungufu uliojitokeza, huku ikihoji sababu ya
mwekezaji huyo kuja na mtaji wa Sh150,000 tu.
Wakizungumza
katika kikao cha kamati hiyo kilichoketi eneo la Mlimani City jijinj
Dar es Salaam leo Januari 18 wajumbe wa PAC walikosoa pia gawio la
asilimia 10 la mapato yote kwa mwaka ambapo Mlimani City wamekuwa
wakikata gharama zao kabla ya kulipa.
Jambo la tatu lililolalamikiwa ni umri wa mkataba ambapo UDSM imetaka upunguzwe kutoka miaka 50 hadi miaka 35.
Mbunge wa Magomeni (CCM) Zanzibar, Jamal Kassim amehoji sababu za chuo hicho kumpokea mwekezaji akiwa na mtaji wa Sh150,000.
"Ukisoma
mkataba huu utaona mtaji wa mwekezaji ni Sh150,000 yaani Dola 75. Maana
yake mwekezaji hakuja na pesa bali alichukua pesa za upangishaji na
kuzifanya kuwa mkopo na anajilipa riba ya mabilioni ya fedha," amesema
Kassim.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka amehoji: "Je, Chuo kikuu cha Dar es
Salaam kilimkubalije mwekezaji mwenye mtaji wa Dola 75 tu? Dhamana
ilikuwa nini?"
Hoja
hiyo ilimwibua Mbunge wa CCM (Vijana) , Khadija Naasir akihoji sababu
ya mwekezaji huyo kutuma barua pepe kila anapotakiwa kutoa maelezo na
UDSM.
Mbunge
wa Ulanga Magharibi Dk Haji Mponda amesema mkataba huo ni mbovu kwa
sababu umeshindwa kuna ardhi iliyopangishwa bila kutumika kwa muda
mrefu.
Baada
ya hoja za wabunge hao, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Hilal Aeshi
ameitaka kamati kuwaita watumishi wa UDSM walioshiriki kusaini mkataba
huo ili wahojiwe na kuchukulia hatua.
"Kwa
kuwa waliotia saini mkataba huo wapo, tuwaite Dodoma, wajieleze ili
wachukuliwe hatua na Rais. Mimi nilikuwa mjumbe wa kamati ya madini ya
Spika, tuliwaita waliohusika wakajieleza," amesema Aeshi.
Hata hivyo baadhi ya wabunge walitaka viongozi wa sasa wa UDSM wajieleze kabla ya kuwaita wa zamani.
Tofauti
na mtazamo wa wabunge hao, Naibu Makamu mkuu wa chuo hicho
anayeshughulikia utawala, Profesa David Mfinanga amekiri kuwa mkataba
huo una mapungufu na kwamba wana mgogoro na Mlimani Holding.
Mwanasheria wa Chuo hicho, Profesa Bonaventure Rutinwa amesema tangu alipoteuliwa alianza kuupitia mkataba huo.
"Tangu
nilipoteuliwa mwaka jana nilifika ofisini kwa Profesa Rwekaza Mukandala
nikamuomba vipaumbele vitano vya kisheria, mojawapo akaniambia ni
kuupitia mkataba wa Mlimani," amesema Profesa Rutinwa.
Akifafanua
zaidi, Kaimu Katibu wa Baraza la Chuo hicho, Dr Saudin Mwakaje alikiri
kuwepo tatizo la mtaji na kwamba walishaiambia kamati hiyo.
Awali
Mkurugenzi wa mipango na maendeleo wa chuo hicho, Pancras Pujuru
amesema Mlimani Holding iliingia mkataba huo mwaka 2004 ukiwa katika
sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza ulihusu kati yake na UDSM na sehemu
ya pili ilikuwa kati yake na Serikali kupitia kituo cha
0 comments:
Chapisha Maoni