Taasisi
ya Msaada wa Kijamii Tanzania (TSSF) imesitaka wanafunzi waliokosa
mikopo ya elimu ya juu kujitokeza kuomba ufadhili wanaoutoa kwa riba
nafuu.
Zaidi
ya wanafunzi 50,000 hawatanufaika na mikopo hiyo kwa ajili ya
kufanikisha kusoma katika vyuo vya elimu ya juu kwa mwaka 2017/18.
Lakini
taarifa iliyotolewa jana na mkurugenzi mkuu wa TSSF, Donati Salla
inasema wanufaika ni wanafunzi wanaoendelea na masomo ngazi ya shahada
na stashahada kutoka chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
Pia,
amesema mwanafunzi ambaye ana matarajio ya kujiunga na masomo ya
shahada ya kwanza mwaka wa masomo 2017/18 naye anaruhusiwa kutuma maombi
ya mkopo huo.
Taarifa
hiyo inasema mwombaji lazima awe na mdhamini ambaye ni mtumishi wa umma
mwenye sifa ya umri wa kudumu kazini kwa kipindi kisichopungua miaka
mitano kabla ya kustaafu.
“Umri
huo unahesabiwa baada ya mwanafunzi kumaliza miaka miwili tangu
alipohitimu masomo yake. Kama mwombaji ni mtumishi wa umma anaweza
kujidhamini mwenyewe,” alisema Salla.
“Mwombaji
ni lazima awe ni mwanafunzi anayeendelea au anayetarajia kujiunga na
taasisi ya elimu ya juu ambayo ipo ndani ya mipaka ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, na mkopo huu ni maalumu kwa wanafunzi ambao hawana
mkopo kabisa,” alifafanua.
Alisema
mwombaji asiye na mdhamini mwenye sifa hizo, atapaswa kulipa ada ya
dhamana ya mkopo atakayopewa na TSSF ambayo ni asilimia mbili ya mkopo
kwa mwombaji ambaye atapata mkopo chini ya Sh4 milioni au asilimia 3 ya
mkopo utakaoanzia Sh4 milioni.
Mkurugenzi
mkuu huyo alifafanua aina za mikopo akisema TSSF inalipa gharama zote
za mafunzo ya elimu ya juu kuanzia mwaka wa kwanza mpaka wa mwisho
ambazo ni ada, chakula, malazi, vitabu, stesheni, posho ya mazoezi kwa
vitendo na posho ya utafiti.
Alisema
kipaumbele kitatolewa kwa wanafunzi waliokosa mikopo inayotolewa na
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) na baada ya kuwahudumia hao
watawafikiria waliopata mikopo kidogo kutoka HESLB.
Alisema
kutakuwa na mkopo wa nyongeza ambao unagharimia sehemu ya mahitaji ya
mwanafunzi anapokuwa chuoni kuanzia anapoomba mkopo huo hadi anapohitimu
masomo.
“Mkopo
huu ni maalumu kwa wanafunzi ambao wanafadhiliwa na HESLB kwa asilimia
sifuri hadi 50 au analipiwa ada tu bila gharama za chakula na malazi au
kulipiwa chakula na malazi bila ada,” alisema na kuongeza:
“Mkopo
huu unahusu wanafunzi ambao wanatoka familia zenye kipato cha kati
ambao wanaweza kujilipia sehemu ya gharama za masomo ila si zote.
Mwombaji wa mkopo huu anapaswa kuomba hitaji lake moja kwa moja.”
Salla
alisema waombaji wanaweza kutembelea tovuti ya TSSF na kwamba Novemba
30 kutakuwa na mkutano kati ya taasisi hiyo na wakuu wa taasisi za elimu
ya juu utakaojadili masuala mbalimbali, hasa ushiriki wao katika utoaji
mikopo.
==>Ingia <<HAPA>> Kupata Fomu na Maelekezo
==>Ingia <<HAPA>> Kupata Fomu na Maelekezo
0 comments:
Chapisha Maoni