Mbunge
wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe amempa tano Mbunge wa
Singida Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu kuwa ameonyesha uongozi.
Zitto ametoa maoni yake hayo baada ya Nyalandu kuamua kujiondoa CCM na kuachia nafasi yake ya ubunge.
Zitto
ameandika, "Lazaro Nyalandu, umeonyesha uongozi. Kwa namna haki za watu
zinavyovunjwa na uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji roho ngumu
sana kuwa CCM. Umefanya maamuzi sahihi, wakati sahihi na kwa sababu
sahihi. Kila la kheri."
Lazaro
Nyalandu leo ametangaza kujivua nafasi zake ndani ya Chama Cha
Mapinduzi na kuandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kwa
kile alichodai kuwa Chama Cha Mapinduzi na Bunge vimekuwa vikishindwa
kuisimamia serikali na badala yake kutumiwa na serikali jambo ambalo
yeye anaona halina afya katika maendeleo ya nchi na linadidimiza haki
mbalimbali.
0 comments:
Chapisha Maoni