Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam 'limemtupa' rumande Mkurugenzi
wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Kigaila Benson.
Kigaila
anayetuhumiwa kutoa lugha za kichochezi Oktoba 12 katika mkutano wake
na waandishi wa habari, alikutana na kadhia hiyo jana aliporipoti
kituoni kituo kikuu cha kanda hiyo.
Mwanasheria
wa Kigaila, Frederick Kihwelo akizungumza na waandishi wa habari nje ya
kituo hicho leo Jumatatu amesema hatima ya dhamana ya mkurugenzi huyo
itaamuliwa kesho Jumanne.
''Amehojiwa
kwa masaa 3 kuanzia saa 7 hadi saa 10 na amehojiwa kwa makosa
aliyoyafanya katika mkutano wake wa Oktoba 12 na wamekataa kutoa dhamana
labda hadi kesho,'' amesema Kihwelo.
''Lakini makosa yake yana dhamana ila wametueleza wanaoweza kuamua ama kupata dhamana au kukosa hawapo ofisini,"
Mwanasheria
huyo amesema katika mkutano huo alizungumza mambo mengi ikiwamo kupigwa
risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kutekwa kwa Ben
Saanane ambaye ni msaidizi wa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
0 comments:
Chapisha Maoni