Makamu
wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema ipo haja kwa
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
kuangalia uwezekano wa kuondoa kodi ya ongezeko la thamani (Vat) kwa
wawekezaji wa makazi nchini ili kuharakisha upatikanaji wa makazi bora
kwa wananchi.
Balozi
Iddi alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizindua mradi
wa nyumba za makazi unaofahamika kama Hamidu City Park uliopo wilayani
Kigamboni. Mradi huo unatekelezwa na Kampuni ya Orange Tanzania Limited
unalenga kujenga nyumba za kisasa zaidi 1,560.
“Makazi
bora ni haki ya kila Mtanzania hivyo sisi kama Serikali ni wajibu wetu
kila siku kufikiria sera bora zitakazo wawezesha wananchi kufanikisha
hilo,’’ alisema.
Alisema
kuna haja ya Taifa kuwekeza zaidi kwenye mipango miji inayowaunganisha
Watanzania, badala ya ile inayowatenganisha kulingana na vipato.
“Sifa
ya miji mizuri ni pamoja mwingiliano wa makazi kati ya watu wenye
vipato tofauti, hatuhitaji kuwa na miji inayowatenganisha watu,’’
alisisitiza.
Akizindua
nyumba 20 za awali, Balozi Iddi aliipongeza kampuni hiyo kupitia
Mkurugenzi wake mkuu, Hamidu Mvungi kwa uzalendo wake wa kuwekeza katika
taifa lake huku akiahidi kumuunga mkono kwa kununua nyumba moja.
Akizungumzia
mradi huo uliopo kilomita 16 tu kutoka eneo la Feri na kilomita 12
kutoka Daraja la Nyerere, Hamidu alisema unahusisha eneo la zaidi ya eka
130 na utatekelezwa kwa awamu tano tofauti.
“
Awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa nyumba zaidi ya 150 ambazo
zitauzwa kati ya mil 120 hadi mil 370 ,’’ alitaja huku akisifia ubora,
usalama na baadhi ya huduma za kisasa ikiwemo viwanja vya michezo
vitakavyohusishwa katika mradi huo.
Hata
hivyo, aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza kama siyo
kuondoa kabisa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ambayo imekuwa
ikichangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la bei kwenye nyumba za makazi.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa.
0 comments:
Chapisha Maoni