Mbunge
wa Ubungo kupitia tiketi ya CHADEMA, Saed Kubenea leo amefikishwa
katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma na kusomewa shtaka la kumshambulia
Mbunge mwenzake wa CCM, Juliana Shoza nje ya viwanja vya Bunge.
Akisoma
shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James
Karayemaha, Wakili wa serikali Beatrice Nsana amedai kwamba mtuhumiwa
alitenda kosa hilo mnamo Julai 3 mwaka huu.
Hata
hivyo, Mhe. Kubenea ambaye anatetewa na Mawakili watano amekana shtaka
hilo na kuachiwa kwa dhaman hadi hapo kesi hiyo itakapotajwa tena Julai
26 mwaka huu kutokana na upelelezi wake kutokamilika.
0 comments:
Chapisha Maoni