Serikali mkoani Kilimanjaro imeyakamata na kuyazuia malori Kumi yenye tani 163 za mahindi yaliyokuwa yakisafirishwa kinyume cha sheria kwenda nchi Jirani ya Kenya kupitia eneo Tarakea.
Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, - Anna Mgwhira amesema licha ya serikali kupiga marufuku uuzaji wa mahindi nje ya nchi, bado baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakikiuka agizo hilo.
Baadhi ya wakulima wa mahindi waliokamatwa wameiomba serikali kuangalia soko la ndani la mahindi ambalo litampa unafuu mkulima kuuza mazao yake
Sauda Shimbo
Juni 25,2017
0 comments:
Chapisha Maoni