Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘TAKUKURU’ imemkamata mtu aliyekuwa anajifanya Mhandisi wa Jiji kisha kuomba rushwa.
Mkuu
wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Erenst Makale amesema mtu mmoja
anayefahamika kwa jina la James Edward ambaye ni Afisa Mtendaji wa Mtaa
wa Mtakuja amekamatwa na Taasisi hiyo kwa kujifanya Mhandisi wa Jiji
kisha kuomba rushwa ya Tsh. 200,000 kwa Mfanyabiashara.
"Mtumishi
huyu aliomba kwa Mfanyabiashara wa Zana za Kilimo ambaye Zana zake
aliweka kwenye eneo ambalo ni Hifadhi ya Barabara…huyu mtu aka-take
advantage (faida) akaenda kwake akijitambulisha kama Mhandisi wa Jiji.
Akamtaka aondoe Zana zake za Kilimo au ampe Shilingi Milioni Moja.
Katika kujadiliana, wakajadiliana wakashusha mpaka kwenye Laki Mbili.
"Mwananchi
huyu akawa Muungwana akaja Ofisini kwetu. Tukafanya mtego tarehe 13,
mtego huo ukafanikiwa lakini hela ilienda kupokelewa na Bwana Godfrey
Joseph Mwangonda ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkolani. Mtu ambaye
aliomba fedha ni Bwana James Edward Mwasemela ambaye ndiye Afisa
Mtendaji wa Mtaa wa Mtakuja.
"Baada
ya kumkamata tulikuja kubaini vitu vingine vya zaida kwamba mtu huyu
James Edward Mwasemela ni sugu pamoja kwamba ni Mtumishi wa Umma lakini
ameshiriki tena kwenye makosa mengine ya utapeli na kufunguliwa kesi
mbili katika mwaka 2013 na 2016 na baadaye kesi hizo ziliondolewa…” Amesema Erenst Makale.
0 comments:
Chapisha Maoni