Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amepokea Kivuko
cha MV Kazi kutoka kwa Kampuni ya kizalendo ya M/S Songoro Marine
Transport Boatyard ya Mwanza iliyokuwa inafanya kazi ya ujenzi wa Kivuko
hicho mara baada ya ujenzi wake kukamilika.
Akizungumza
na wananchi, Prof Mbarawa jana alisema lengo la Serikali kuongeza
Kivuko hicho ni kuboresha huduma za kusafirisha abiria na magari kati
ya Magogoni na Kigamboni.
“Uwepo
wa vivuko vitatu kutasaidia utoaji wa huduma kwa wakati na kwa urahisi
na ikitokea Kivuko kimoja kimepelekwa kufanyiwa ukarabati huduma
zitaendelea kama kawaida bila kuathiri utaratibu wa kawaida”.Alisema Prof Mbarawa.
Aliongeza
kuwa ili kuendana na kasi ya Mhe. Rais John Magufuli Wizara yake
itaendelea kuboresha huduma za Vivuko katika Mikoa mingine ikiwemo Mkoa
wa Lindi , Kivuko cha Pangani, na Kivuko cha Kigongo Busisi Mkoani
Mwanza.
Nae
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Dkt. Mussa
Mgwatu alisema Kivuko cha MV Kazi kimejengwa kulingana na viwango
vinavyotakiwa Kimataifa na ukaguzi wake umefanywa na Mamlaka ya Udhibiti
wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na kuthibitishwa kuwa ni
salama kwa ubebaji wa abiria na magari.
Ujenzi
wa MV KAZI umegharimu Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo
wa kubeba abiria 800 magari 22 sawa na jumla ya tani 170.
Kivuko
hicho kimekabidhiwa jana kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kati ya
Magogoni na Kigamboni Jijini Dar es salaam na kuongeza idadi ya vivuko
katika eneo hilo kufikia vitatu.
0 comments:
Chapisha Maoni