Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro jana alifanya mazungumzo
na wazee pamoja na viongozi wa dini wilayani Kibiti mkoani Pwani ili
kubaini waalifu wanaotekeleza mauaji ya watu wilayani humo na kusema
vyovyote itakavyokuwa lazima watawarudisha kwenye msitari.
IGP
Sirro alisema kupitia mazungumzo hayo tayari amepata taarifa za
wahalifu hao ingawa ni mapema kuziweka wazi ila amewakikishia wananchi
kuwa waalifu wao ni lazima watapatikana.
“Kubwa
ni kwamba wazee wetu wa Kibiti wametueleza taarifa nyingi sana na
mnavyojua hawa waalifu wanaishi ndani ya Kibiti, ndani ya Ikwiriri, kwa
hiyo wazee wetu wamejaribu kutueleza ni wapi tunaweza kuwapata na chanzo
cha mambo yote haya,” alisema IGP Sirro na kuongeza;
“Kwa
hiyo kimsingi mambo mengine mengi ni ya kipelelezi ambayo siwezi
kuyasema kwa sasa, lakini kikubwa wametupa dira, muelekeo kwa maana
kwamba wale ndugu zetu au maadui zetu kwa lugha nyepesi tumepata njia
nzuri ya kudeal nao. Kwa hiyo nitume salamu kwao kwamba waendelee
kukimbia lakini njia ya muongo ni fupi na mwisho wa siku tutawarudisha
kwenye mstari"
0 comments:
Chapisha Maoni