Suleiman Msuya
IKIWA
ni takribani miezi 10 sasa kwa Chama cha Wananchi (CUF), upande wa
Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad kuvamiwa katika Ofisi Kuu za
Buguruni na kundi la Profesa Ibrahim Lipumba chama hicho kimezindua
ofisi mpya za chama hicho katika eneo la Mtaa wa Idrisa, Kata ya
Mzimuni, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Aidha,
Seif amesisitiza kuwa hatarajii kukutana na Profesa Lipumba kwa kile
alichodai kuwa hatambuliki katika chama na hana sifa hizo kwa sasa.
Akizindua
ofisi hiyo ambayo lengo kubwa ni kwa ajili ya wabunge 40 wa CUF, Seif
alisema uamuzi wa wabunge hao kumpatia ofisi ya kufanyia kazi hapo ni
cha kiungwana na kinahitajika kuungwa mkono na wanachama wote.
Alisema
kwa muda wa miezi 10 sasa wamekuwa wakishindwa kufanya kazi hasa upande
wa Tanzania Bara jambo ambalo limewaathiri sana hivyo kupatiwa ofisi
kutamsaidia kutimiza majukumu yake vilivyo bila hofu yoyote.
Maalim
Seif alisema kukosa ofisi kumewaathiri sana katika baadhi ya mambo
hivyo anaamini kwa sasa akifikia Dar es Salaam anamahali pa kukutana na
wakurugenzi wake.
“Nimekuwa
ni kija hapa nakosa sehemu ya kukutana na wakurugenzi, viongozi
mbalimbali wanachama ila hiki ambacho wabunge wamefanya ni cha kuungwa
mkono sijawahi kufanya kazi na wabunge wanao kipenda chama kama kipindi
hiki,” alisema.
Katibu
huyo alisema atahakikisha kuwa anaanza kazi haraka iwezekanavyo kwa
kukutana na wakurugenzi wake ili waweze kutekeleza majukumu ya chama.
“Hakuna
shaka kuwa huu unaoitwa mgogoro umeturudisha nyuma sana hivyo naamini
wakati wa kufanyakazi umerejea na hawa wabaya wetu hawata ambulia kitu
kwani CUF ni chama imara hakitikisiki,” alisema.
Maalim
Seif alisema jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kukimaliza chama ni kubwa lakini hawataweza kufikia lengo hilo kutokana
na misingi ya chama hicho.
Alisema
kwa sasaa atafanya kazi katika ofisi hiyo ambayo amepewa na wabunge
hadi hapo muafaka wa ofisi kuu Buguruni utakapopatikana huku akisisitiza
kuwa haki haipotei ila inachelewa.
Katibu huyo alisema anaimani na mahakama kuwa ita wapatia haki stahiki hivyo kuwataka wanachama kuendelea kuwa na subira.
Aidha,
alisema kupitia mgogoro huo hadi sasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa nchini inashikilia zaidi ya sh. bilioni 1.2 ambazo ni ruzuku ya
chamahicho.
Maalim
Seif alisema fedha hizo ni pamoja na zile ambazo ofisi ya msajili
ilimpatia Lipumba hivyo waamini mgogoro ukiisha wata pata haki yao.
Kwa
upande mwingine Katibu huyo alisema hana mpango wa kukutana naLipumba
kuhusu mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho kwa kile alichodai kuwa
si kiongozi wala mwanachama wa chama hicho.
Alisema CUF haimtambui Lipumba kwa sifa yoyote tofauti na kumfukuza uanachama hivyo yeye hawezi kukukutana na mtu kamahuyo.
Maalim Seif alisema pamoja na kuwa hawamtambui Lipumba kama kiongozi au mwanachama ila akiomba msamaha wapo tayari kumsamehe.
Akizungumza
baada ya kuzinduliwa ofisi hizo Mbunge wa Viti Maalum na Kiongozi wa
Wabunge wa CUF bungeni, Riziki Ngwali alisema wamelazimika kufungua
ofisi nyingine ili wapate mahali pa kukutana wakiwa nje ya Bunge.
Ngwali alisema kupitia ofisi hiyo wataweza kujadiliana mambo mbalimbali yanayo wahusu wabunge na wananchi na kuja na ufumbuzi.
Kwa
upande wake Mbunge wa Temeke CUF, Abdallah Mtolea alisema katika ofisi
hiyo wanatarajia kuajiri wataalam mbalimbali ambao watasaidia kufanya
tafiti na kupitia tarifa mbalimbali za Bunge ili kuwarahisishia katika
uchangiaji bungeni.
Alisema
katika ofisi hizo wameingia mkataba wa kulipa sh. milioni 18 kwa mwaka
ambazo zitatolewa na wabunge wenyewe kwa maslahi ya chama chao.
0 comments:
Chapisha Maoni