Sakata
la watumishi wa umma waliofanyiwa uhakiki wa vyeti limezidi kuchukua
sura mpya kila iitwapo leo ambapo awamu hii, Waziri wa serikali ya awamu
ya tano amebainika kuwa miongoni mwa watumishi ambao vyeti vyao vina
utata.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi
ametajwa katika orodha ya watumishi ambao vyeti vyao vina matatizo
ambapo uhakiki wake ulifanyika wakati akiwa mkufunzi katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM), kabla ya kuteuliwa kuwa mbunge na kisha
waziri.
Waziri
Prof. Kabuni ambaye amebobea katika sheria, pamoja na waafanyakazi
wengine wa UDSM wametajwa katika orodha ya watumishi wa umma ambao vyeti
vyao havijakamilika.
Katika
orodha aliokabidhiwa Rais Dkt Magufuli na Waziri wa Nchi, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, jumla ya
watumishi 9,932 walikutwa na vyeti vya kughushi, huku wengine zaidi ya
1,500 wakiwa na vyeti vyenye utata na wengine walikuwa wamepeleka vyeti
pungufu kwenye uhakiki.
Akizungumza
suala hilo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.
Mukandala alisema kwa Prof. Kabudi ametajwa katika orodha hiyo kwa
sababu cheti chake cja kidato cha nne hakikuonekana wakati wa uhakiki.
Aidha, Prof. Mukandala alisema kuwa tayari Prof. Kabudi ameshawasilisha
cheti hicho na kwamba watakipeleka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA)
kwa ajili ya uhakiki.
Wakati
Rais Magufuli akikabidhiwa ripoti ya uhakiki wa watumishi wenye vyeti
feki alisema kuwa, kwa wale ambao wanavyeti pungufu, wanaendelee kubaki
kazini lakini uhakiki ufanyike vizuri kwa sababu si kila mtu alipita
kidato cha sita kiweza kufika chuo. Hivyo kama hakupita kidato cha sita
alafu ukamwambia akuletee cheti, hatokuwa nacho.