Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati akizungumza kwenye kongamano na kilele cha maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika kitaifa Itigi wilaya ya Manyoni.
Alisema kumekuwa na tatizo la uhaba wa wauguzi na watumishi wengine wa kada zingine za afya, tatizo hili limezidi kuwa kubwa, baada ya hatua zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya tano kuondoa watumishi hewa na wenye vyeti feki.
“Wauguzi pia wapo waliokubwa na hatua hii na kusababsisha uhaba wa wauguzi kuwa mkubwa zaidi. Nimearifiwa kuwa kuna baadhi ya vituo vya afya vimefungwa kwa kukosa watumishi baada ya zoezi hili. Hata hivyo, Rais Dk. Magufuli ameagiza nafasi za ajira, zitangazwe ili kujaza nafasi hizo mapema iwezekanavyo,” alisema Waziri Ummy.
Hata hivyo, alisema wizara itatoa kipaumbele kwa mikoa iliyo na uhaba mkubwa ikiweo mkoa wa Singida pamoja na hospitali zake teule ikiwa ni pamoja na hospitali ya St. Gasper iliyopo Itigi.
Aidha, Ummy alisema wizara itatoa mwongozo wa zamu za wauguzi ili kuwe na ratiba ya utaratibu mzuri kama inavyofanyika katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Akisisitiza, alimwagiza katibu mkuu katika wizara yake aweke mkakati unaotekelezeka kuhakikisha kuwa wanapatikana wauguzi wengi waliobobea katika maeneo mbalimbali ya utoaji wa huduma za kiuguzi na ukunga.
“Pia ahakikishe kuwa vyuo vyetu vilivyokuwa vinatoa mafunzo ya stashahada ya juu viweze kuandaa mitaala kwa mujibu wa miongozo iliyopo, ili vizalishe wauguzi wa kati waliobobea. Nimeaambiwa kundi hili lilikuwa la msaada mkubwa, kwa sasa hatulizalishi, kwa kuwa walimu vyuoni imekuwa tatizo,” alisema.
Katika hatua nyingine, waziri huo ameahidi kwamba watafuatilia kwa karibu tukio lililotokea mkoani Arusha wilaya ya Loliondo la muuguzi kupigwa wakati akitekeleza wajibu wake ili wahusika waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki.
Maadhimisho hayo ni kukumbuka ya mwassisi wa taaluma ya uuguzi Florence Nightngale aliyezaliwa Mei, 12 mwaka 1820. Wakati wa sherehe hizi, huwa mishumaa inawashwa kama ishara ya upendo na utumishi bora moyoni mwa muuguzi. Muasisi huyu, ndiye aliyefungua chuo cha kwanza cha uuguzi nchini Uingereza.
Florence aliyeanza kutoa huduma ya afya mwaka 1844, mwaka mmoja baadaye kulitokea vita na yeye akawa nahudumia majeruhi kwa kutumia mishumaa nyakati za usiku kwa vile hapakuwepo na nishati y yote wakati huo, kwa huduma yake hiyo ya kutibu majeruhi wa vita,aliweze kupunza vifo kutoa asilimia 42 hadi asilimia mbili.
Pia wauguzi waliokuwepo kwenye maadhimisho hayo kutoka mikoa mbalimbali nchini, walirudia kiapo chao,“Naapa mbele ya Mungu na mbele ya mhadhara huu, kuendesha maisha yangiu,na kutekeleza wajibu wangu wa kazi kwa uaminifu. Sitafanya vitendo vyo vyote vile vilivyo viovu na sitochukua au kutoa dawa ye yoter ile ninayoifahamu kuwa ina madhara,” sehemu ya kiapo.
Awali wauguzi, viongozi mbalimbali wa serikali na madhehebu ya dini pamoja na wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo, walisimama kwa dakika moja kuwakumbuka na kuwaombea wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa shule ya Lucy Vicent waliopoteza maisha yao kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea hivi karibuni.