Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ametangaza vita kwa
watumishi wanaoruhusu uingizwaji wa bidhaa bandia nchini, na kutoa onyo
kwamba watakao fanya hivyo wajiandae kuondoka.
Mwijage
ametoa onyo hilo juzi Bungeni mjini Dodoma, wakati akisoma bajeti ya
wizara yake, ambapo pia alipiga marufuku bidhaa bandia kuingia nchini
kutoka nje ya nchi kuanzia Julai mosi mwaka huu.
“Ikifika
mwezi Julai mwaka huu, kama bidhaa feki zikipita kuingia nchini mtakuwa
hamnitakii mema, na walio chini yangu mkae kabisa mkao wa kuondoka kama
bidhaa zisizokidhi viwango zitapia na kuja kuumiza viwanda vyetu
nchini,” alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni