Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewasamehe
wafanyakazi tisa wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) waliokuwa
wamesimamishwa kazi kwa kosa la kurusha habari ya uongo kumhusu kiongozi
huyo wa nchi.
Wafanyakazi
hao walisamishwa kazi mwezi Machi kwa kuhusika katika makosa ya
kiweledi na kiuhariri yaliyosababisha kutangazwa kwa taarifa ambayo
haikuwa sahihi Machi 03, 2017.
Wafanyakazi
hao walirusha hewani taarifa ya uongo iliyosambazwa na mtandao wa Fox
Channel.com kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump amesifu utendaji kazi wa
Rais John Pombe Magufuli na kwamba ni mfano mzuri wa kuigwa Afrika.
Taarifa
iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayub Rioba, ilieleza kuwa
makosa hayo yalileta usumbufu kwa umma na yasingefanyika endapo taratibu
zote za kitaalamu zingefuatwa kuthibitisha ukweli wa taarifa yenyewe.
Watangazaji
waliotangaziwa msahama huo ni Rais Dkt Magufu ni pamoja na Gabriel
Zackaria, Elizabeth Mramba, Prudence Constantine, Dorothy Mmari,
Ramadhani Mpenda, Leya Mushi, Alpha Wawa, Chunga Ruza na Judica Losai.
Rais
Dkt Magufuli alitoa msamaha huo alipofanya ziara katika kituo hicho
jana ili kuangalia utendaji kazi pamoja na kuzungumza na wafanyakazi
kuweza kutambua changamoto zinazowakabili.
0 comments:
Chapisha Maoni