Rais
Dkt Magufuli ameshindwa kujizuia na kusema kuwa amekumbwa na majonzi
makubwa baada ya kuona majeneza 35 ya wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent
ya jijini Arusha waliofariki katika ajali ya basi wilayani Karatu
Mkoani Arusha.
Rais
Magufuli ameyasema hayo wakati miili ya wanafunzi 35, walimu 2 na
dereva mmoja ikiagwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na
kisha kusafirishwa maeneo mbalimbali kwa ajili ya maziko.
Kupitia
ukurasa wake wa Twitter, Rais Dkt Magufuli aliandika, “Nimepatwa na
uchungu na majonzi makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao
waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha .”
“Tumewapoteza mashujaa wetu ktk elimu. Tuwaombee na tuendelee kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu 2/2.”
Aidha,
Rais Dkt Magufuli amewasihi wa Tanzania kuendelea kuwa wamoja wakati
wakiomboleza tukio hili kubwa lililoikumba nchi na kuacha simanzi
miongoni mwa watu wengi.
“Tunapoomboleza vifo vya wapendwa wetu tuendelee kuwa wamoja. Mungu ibariki Tanzania.”