Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba bungeni leo amesema serikali
bado haina sheria ya kuthibiti matumizi ya kilevi aina ya shisha ila
lipo agizo la Waziri Mkuu la kupiga marufuku biashara hiyo na kutaka
agizo hilo lifuatwe na kila mtu.
Mwigulu
Nchemba amesema hayo wakati akijibu swali bungeni kuhusu matumizi ya
kilevi hicho cha shisha ambacho bado katika baadhi ya maeneo kimeendelea
kutumika na kuleta athari kwa watumiaji.
"Ni
kweli serikali baada ya kuona matumizi ya kilevi cha Shisha yanaleta
athari kwa binadamu, serikali imeanza kuweka sheria za kuthibiti
matumizi ya shisha, usambazaji wa shisha na uagizaji wa kilevi hicho,
lakini wakati tunasubiri sheria hizo tunatambua kuwa lipo agizo la
Waziri Mkuu la kupiga marufuku matumizi ya kilevi cha shisha ambalo
utekelezaji wake ulianza mikoani kama Dar es Salaam, Mbeya, Iringa na
mikoa mingine imeendelea kuitikia. Kwa hiyo maelekezo ya Mh. Waziri Mkuu
yanafanyiwa kazi bila kupunguza hata nukta" alisema Mwigulu Nchemba
Mbali
na hilo Waziri Mwigulu alisema anatambua wapo watu walipewa leseni kwa
ajili ya kufanya biashara hiyo ya shisha lakini kwa kuwa serikali
inajali masuala ya afya ya Watanzania ndiyo maana wanatakakuja na sheria
ili kuthibiti kilevi hicho ambacho kina athari kwa watumiaji.
0 comments:
Chapisha Maoni