Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles Mkumbo amesema
wanamshikilia mmiliki wa basi dogo aina ya Coaster ambayo ilipata ajali
na kusababisha vifo kwa wanafunzi, walimu na dereva wa shule ya siku ya
Lucky Vincent Jumamosi huko Karatu, Arusha.
RPC
Mkumbo amedai wanamshikilia mmiliki wa shule hiyo kwa kuruhusu gari
yake hiyo kubeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wa gari
"Siku
ya tukio walikuwepo abiria 38 kwenye gari katika uchunguzi baada ya
kubaini hilo tumeshachukua hatua kwa mtu aliyewezesha gari hilo kupakia
hao watu, tumeshamkamata mmiliki wa gari ambaye ndiye mwenye shule hii,
sasa hivi tunaendelea na uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa
mahakamani" alisema RPC wa Arusha
Kwa
mujibu wa Mkumbo anasema gari hiyo ilikuwa na kibali cha kubeba watu 30
lakini gari hiyo siku ya ajali ilikuwa na watu zaidi ya 30.