Marekani
imesema kuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika jaribio lake la
kwanza la mtambo wa kutungua makombora ya nyuklia ya masafa marefu.
Mtambo
huo wa ardhini umefungwa katika kambi ya kijeshi iliyopo Califonia
kwaajili ya kujihami na vitisho ambavyo vimekuwa vikitolewa na maadui
zake ikiwemo Korea Kaskazini.
Aidha,
Pentagon imesema kuwa jaribio hilo limefanyika baada ya Korea Kaskazini
kufanya majaribio yake ya makombora tisa ya masafa marefu mwaka huu
hivyo kutishia usalama wa nchi hiyo.
“Mfumo
huu ni mhimu sana kwa ulinzi wa taifa letu na jaribio hili ni
uthibitisho mkubwa kwamba tuna uwezo wa hali ya juu wa kujilinda na
kutetea usalama wa raia wetu,” amesema Mkurugenzi wa kitengo cha ulinzi
wa makombora, Admirali Jim Syring.
0 comments:
Chapisha Maoni