Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
anatarajia kufanya ziara rasmi ya siku tatu kuanzia tarehe 05 Juni,
2017 Mkoani Mara.
Kwa
mujibu wa ratiba ya Mkoa, Mhe Samia atatembelea Wilaya ya Tarime,
katika Kituo cha Afya cha Nyamwaga kinachojengwa na wananchi kwa msaada
wa Mgodi wa Acacia North Mara.
Pia,
Mhe. Makamu wa Rais atapata fursa ya kutembelea Bonde la Mto Mara
kunakokusudiwa kuanza kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari.
Mchana siku hiyo hiyo atafanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha
Bisarwi; katika eneo hilo kunakusudiwa kujengwa kiwanda cha sukari.
Aidha
tarehe 6/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais ataenda Wilaya ya Serengeti ambapo
ataweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Wilaya; mchana atafanya
Mkutano wa Hadhara katika Uwanja wa Mbuzi, Mugumu mjini.
Tarehe
7/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais atakuwa Musoma ambapo ataweka jiwe la
msingi kwenye barabara ya km. 9.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami
katika Manispaa ya Musoma. Pia atatembelea kiwanda cha Samaki cha Musoma
Fish Processors (T) Ltd na kufanya Mkutano wa Hadhara katika uwanja wa
Mukendo Musoma Mjini.
Hii ni mara ya kwanza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa na ziara rasmi Mkoani Mara.
0 comments:
Chapisha Maoni