Waziri
wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuanzia sasa
mtu yoyote atayeweza kupata majeraha yasiyokuwa na utata wapewe matibabu
kwanza hospitali bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Jeshi la Polisi
(PF3) kama ilivyozoeleka.
Mwigulu
ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii Facebook kwa kusema
utaratibu huo unajicho la karibu kutoka kwenye vyombo vya usalama ili
kubaini ukweli wa jeraha la muhusika.
"Tumeamua
majeruhi, mahututi asiyeweza kutoroka na mtu mwenye majeraha yasiyo na
utata wapewe matibabu kwanza bila PF3..Hatua za kufuata PF3 zianze mara
moja wakati akiendelea kupewa matibabu, hii tunalengea kuokoa maisha yao
kwanza, utaratibu huu unajicho la karibu kutoka kwenye vyombo vyetu vya
usalama ili kubaini ukweli jeraha la mhusika". Ameandika Mwigulu
Mwigulu
amesema hayo baada ya Jeshi la Polisi kutupiwa lawama nyingi kutoka kwa
wananchi walipatwa na matatizo kushindwa kupewa huduma hospitali kwa
haraka mpaka wapitie kituo cha Polisi kupatiwa cheti cha PF3 ili aende
kupata huduma.
0 comments:
Chapisha Maoni