Chama cha mapinduzi (CCM) leo May 25
2017 Dar es salaam kimezungumza na Waandishi wa habari kupitia kwa
Katibu wake wa itikadi na uenezi Humphrey Polepole na kuzungumzia mambo
mawili makubwa yanayoendelea.
JAMBO LA KWANZA: ‘Leo nitazungumza
mambo mawili ambayo yamekua makubwa na yanaendelea kwenye taifa letu,
moja ni swala la ulinzi na usalama wa Wananchi wetu wa Tanzania hasa
zaidi katika muendelezo wa matukio kwenye eneo la Mkuranga, Kibiti na
Rufiji‘
‘Sisi kama chama tumelifuatilia na kuona ni vyema kusimama na
Watanzania wakiwemo Wanachama wa CCM katika maeneo haya kusema tuko
pamoja, tunatambua wanapitia wakati mgumu, wapo waliopoteza maisha sio
kwasababu ya mapenzi ya Mwenyenzi Mungu… wamepoteza maisha yao kwasababu
yamekatizwa’
"Sitaki kusema maneno makubwa kwamba zaidi kwamba ikiendelea
tutapenda kuona watu wengine wanawajibishwa.. niseme pia tumesikitishwa
sana, sisi tunaamini demokrasia ya vyama vingi ni mshikamano lakini
tunahisi kama tumeachwa wenyewe, tumevunjika moyo sana, ukimya wa
wenzetu vyama vingine vya siasa umetusikitisha"
“Nimeona wenzangu wametingwa na kufanya siasa za madaraka kuliko
siasa za maendeleo na zinazohusika na shida za watu wetu, hakuna namna
nyingine nzuri ya kuwahudumia Watanzania kama kushikamana wakati wa
matatizo bila kujali tofauti zetu za kiitikadi" – Polepole
JAMBO LA PILI: "Nalisema hili katika namna ambayo mara
nyingi watu wamezoea na ni mazoea mabaya kwamba mtu akifanya jambo jema
hatakiwi kusifiwa sababu ni wajibu wake, leo napenda niwaambie
kivingine… jambo ambalo Rais Magufuli amelifanya jana ninawaomba kwa
heshima kubwa Watanzania wote tumuunge mkono"
"Vita zipo za aina nyingi, zipo tunazopigana kwa silaha… mtu na mtu,
nchi na nchi… wengi wamezoea hizi…. lakini zipi vita za kiuchumi, ni
mbaya zaidi kuliko vita ya kupigana na silaha, inalenga kuturudisha
nyuma na kufukia malengo ya sisi kuwa taifa huru na linalojitegemea"
"Nawaomba Watanzania sio tu WanaCCM kwa heshima kubwa tumuunge mkono
Rais wetu mpendwa, atakua imara na madhubuti zaidi tukisimama nae sote"
0 comments:
Chapisha Maoni