Skip to content
Masaa kadhaa baada ya kuiongoza timu yake ya Simba SC kurejea
katika anga ya kimataifa kwa ushindi wa kombe la Azam Sports Federation
Cup dhidi ya Mbao FC, kiungo wa Simba Jonas Mkude ameripotiwa kupata
ajali mbaya akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea Dodoma.
Nahodha
huyo wa Simba amepata ajali hiyo maeneo ya Mitibora, Dumila mkoani
Morogoro akiwa njiani kurejea Dar es Salaam kuiwahi Taifa Stars. Taarifa
za awali zinasema ameumia maeneo ya shingoni, amekimbizwa kwenye
hospitali ya mkoa wa Morogoro pamoja na majeruhi wenzie ambao baadhi
wana halimbaya.
Kwenye gari ambayo Mkude amepata nayo ajali walikuwepo watu 6, na
kilichopelekea ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi la nyuma. Majeruhi mmoja
yuko mahututi.

Tutaendelea kujuzana hali yake na majeruhi wengine kadri taarifa zitakavyokuwa zinatoka.
Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
xxxxxxxxxxxxx
0 comments:
Chapisha Maoni