Mwanasheria
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Tundu Lissu,
amesema ameanza kuogopwa na viongozi wa serikali baada ya jina lake
kuwa miongoni mwa majina matano bora ya wagombea wa nafasi ya urais
katika Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kutokana na misimamo yake
ya kuitetea Katiba ya Tanzania.
Akizumgumza
na waandishi wa habari Mwanza jana, Lissu alisema tangu atangaze nia
yake ya kugombea urais wa TLS ameanza kuogopwa kutokana na kujulikana
kwa misimamo yake kuhusu masuala ya sheria, siasa na katiba ya
nchi hii.
Alisema
TLS ina majukumu makubwa katika nchi ya kulinda utawala wa sheria na
wanasheria ndiyo wanaojua kuliko mtu yeyote zinapotungwa sheria mbovu
na zile za kikandamizaji, pia wao ndiyo wanapaswa kuwa wa kwanza kuanza
kuzipigia kelele sheria hizo.
“Kwa
miaka mingi TLS imeongozwa na watu ambao hawafikiri kwamba wajibu wao
wa kwanza kulinda utawala wa sheria, wao wanafikiri wajibu wao wa
kwanza ni kuwapendeza wanasiasa na matokeo yake TLS imepotea,
wanachoogopa ni kwamba hii raha ambayo wameipata miaka yote hii wakati
wanasheria wa TLS wakiwa usingizini akija huyu Lissu itaisha,”
alisema Lissu.
Alisema
aligombea nafasi hiyo baada ya kumsikia Rais Dk. John Magufuli
akizungumza mbele ya watanzania kwamba wakili yeyote atakayewatetea
watuhumiwa wanaokutwa na dawa ya kulevya au nyara za serikali wakamatwe
na kuwekwa ndani.
Alisema
aliposikia kauli hiyo alicheka na kusema sasa ni wakati wa yeye kuwa
rais wa TLS ili kauli za aina hiyo zikome na siku mbili kabla ya Rais
Dk. John Magufuli kutoa kauli hiyo, Bunge lilipitisha sheria ya msaada
wa sheria.
“Sheria
hiyo inasema mtu yeyote anayefunguliwa kesi ya jinai, au madai kama ni
maskini hana uwezo wa kumlipa wakili atapatiwa huduma hiyo na wakili
atalipwa na mtendaji mkuu wa mahakama.
“Sheria
hiyo inampatia haki mwananchi yeyote atakayekuwa na kesi ya mauaji,
pembe za ndovu au dawa za kulevya kupata wakili atakayelipwa na
serikali.
“Siku
mbili baadaye Rais anakinzana na sheria hiyo nilishangaa kweli. Tayari
sheria hiyo imetungwa ni jambo muhimu kweli kwa sababu katika nchi
hii watu wanasingiziwa sana, kwenye maegereza nyingi nchini wamejazana
wananchi ambao hawana hatia na wapo huko kwa sababu hawakuwa na
mawakili wa kuwatetea,” alisema Lissu.
Lissu alisema endapo atachaguliwa kuwa rais wa TLS atahakikisha sheria ya msaada wa sheria inatekelezwa.
Kuhusu
hoja ya Waziri wa katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe ya
kutishia kukifuta chama hicho hicho kwa kuwa kimeanza kujiingiza katika
masuala ya siasa, Lissu alisema wanaoleta hoja za kutaka kukifuta chama
hicho kama ni wanasheria ujuzi wao wa sheria ni wa shaka lakini kama ni
wasiojua sheria wanasamehewa.
Alisema
sheria ya iliyoanzisha TLS inasema mwanachama yeyote aliyekidhi vigezo
vya chama hicho ana haki ya kuwa mgombea wa nafasi yoyote ya uongozi na
haijasema ukiwa mwanachama wa chama chochote cha siasa unapungukiwa
sifa ya kugombea.
“Watu
wanazungumza kana kwamba ni makosa mwanasheria kuwa mwanasiasa,
katika nchi hii katiba imeruhusu siasa za vyama vingi, kuwa
wanachamaau kiongozi wa chama.
“Kuwa
tu mwanachama una kuwa na fursa ya kugombea nafasi mbalimbali za
uongozi serikalini lakini sasa watu wanataka kuaminishwa kuwa ukiwa
mwanasiasa huna haki,” alisema