Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kuuarifu umma kuwa, uhakiki wa ubora wa wanafunzi wa elimu ya juu
hufanyika kwa mujibu wa Kifungu 5(1)(b)(c) cha Sheria ya
Vyuo Vikuu Sura ya 346 ya Sheria za Tanzania.
Katika kutekeleza jukumu hili Tume ilianza zoezi la uhakiki kuanzia mwezi Agosti 2016. Hadi kufikia Februari 2017 zoezi
Hii
ni mara ya kwanza uhakiki wa sifa za wanafunzi wa vyuo vyote nchini
kufanyika kwa wakati mmoja. Lengo la uhakiki lilikuwa kujiridhisha
kuwa wanafunzi waliopo vyuoni ni wale waliodahiliwa kwa mujibu wa
sheria na taratibu na kwamba wanakidhi vigezo stahiki.
Uhakiki
ulifanyika kwa kulinganisha taarifa za TCU na zile zilizowasilishwa na
vyuo. Uhakiki huo ulihusisha jumla ya wanafunzi 131,994 waliopo vyuoni
kwa mwaka wa masomo 2016/17.
Baada
ya kulinganisha orodha zilizowasilishwa na vyuo na ile ya TCU
ilibainika kuwa wanafunzi 123,827 sawa na asilimia 93.8 wana sifa stahiki. Aidha jumla ya wanafunzi 8,167 sawa na asilimia 6.2 tu walibainika kuwa na kasoro katika taarifa za sifa zao.
Kufuatia
hali hiyo, Tume ilitoa taarifa kwa umma kuwaomba wanafunzi kurekebisha
dosari hizo kwa kuthibitisha taarifa zao kupitia vyuo husika ifikapo
tarehe 28 Februari 2017 ili kuweka kumbukumbu sahihi za mwanafunzi.
Hata
hivyo imebainika kuwa taarifa hiyo imepokelewa kwa mtazamo na hisia
tofauti na hivyo kusababisha mkanganyiko vyuoni. Umma unaarifiwa kwamba
haikuwa nia wala lengo la Tume kusababisha mkanganyiko huo.
Kwa
kuwa uhakiki wa sifa za wanafunzi ni kazi endelevu ya Tume na kutokana
na maombi ya wadau mbalimbali, Tume sasa itaendelea kuwasiliana moja
kwa moja na vyuo katika kukamilisha zoezi hilo.
Hivyo wanafunzi wote waliokuwa wameorodheshwa katika taarifa iliyotolewa awali wanaombwa kuwa watulivu na kuendelea na masomo yao kama kawaida.
Hivyo wanafunzi wote waliokuwa wameorodheshwa katika taarifa iliyotolewa awali wanaombwa kuwa watulivu na kuendelea na masomo yao kama kawaida.
Aidha
ifahamike kuwa wanafunzi waliokuwa wameorodheshwa siyo kwamba
wamethibitika kuwa hawana sifa stahiki bali kuna dosari katika taarifa
zao. Ndiyo sababu Tume iliwaomba kuthibitisha taarifa zao ili kuondoa
dosari hizo.
Imetolewa na
Kaimu Katibu Mtendaji
24 Februari 2017