Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya nyumbani kwake
Upanga jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya alikuwa
amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa
matibabu mpaka aliporuhusiwa kurejea nyumbani kwake mara baada ya
kupata nafuu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimuombea Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumaliza
mazungumzo yao nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali
nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya akimsindikiza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alifika nyumbani
kwake Upanga kwa ajili ya kumjulia hali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali
nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU