Mbunge
wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi
Kabwe jana alijificha ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma kwa hofu ya
kukamatwa na Jeshi la Polisi mara tu atakapotoka nje ya ukumbi huo.
Zitto
Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika kuwa Polisi wa bunge
wamemwambia kuwa watamkakata kwa kosa la uchochezi ambalo yeye mwenye
hafahamu ni lipi
Akizungumzia taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa amesema si kweli kwamba Polisi walikuwa Bungeni kumsubiri Zitto atoke wamkamate.
“Hiyo taarifa yeye mwenyewe ndio anajitangazaia akamatwe lakini sisi hatumkamati kwasababu hatuna ishu nae
“Unajua
watu wanafikia mahali wanatafuta umaarufu wakamatwe ili wapige mayowe…
hatuna mpango wowote wa kumkamata kwasababu hajatenda kosa la jinai” Amesema Kamanda Mambosasa.