Wachawi wana uwezo wa kumtia mtu nuksi na mikosi mbalimbali.
Nuksi
na mikosi hiyo inaweza kuja katika sura ya magonjwa na maradhi
sugu yasiyopona kama vile kisukari, ukimwi, ugumba, mimba
kuchoropoka, kifafa nakadhalika.
Kufukuzwa kazi, matatizo katika ndoa, ajali, umasikini, vifo na misiba mfululizo, kuchukiwa na watu nakadhalika.
Zipo
njia mbalimbali wanazo tumia wachawi katika kuwatia watu nuksi
na mikosi, Katika makala ya leo, nitaelezea njia moja wapo kama
ifuatavyo:
Katika njia hii, wachawi wakitaka kumtia mtu mikosi, hufanya mambo yafuatayo :
i. Wanachukua hela ambayo haitumiki
ii. Wanachukua mavi ya mbwa mweusi ambayo ameyanya usiku wa manane
iii.Wanachukua
mkaa ulio kwisha tumika, ambao umetumika mahali ambapo watu
hawalali kama vile kilioni au kwenye baa na migawaha inayo kesha
lakini mara nyingi, huchukua mkaa wa kilioni.
iv.Wanachukua
mavi ya ndege anaitwa Mumbi. Huyu ndege aitwae Mumbi
anapatikana porini. Anafanana sana na bata na ana puyanga la
rangi nyekundu.
v. Wanachukua shahidi la kaburini pamoja na ndumba zingine za kichawi
vi.
Wanachukua kitu chochote cha mtu aliye kusudiwa kutiwa mikosi
kama vile jina lake, picha yake, mchanga alipokanyagia, mate,
kucha, au chochote kile.
Baada
ya hapo, mchawi huyo atakwenda kaburini usiku wa manane na
kuvizika vitu vyote nilivyo vieleza hapo juu, huku akisema
maneno ya kichawi. Basi mtu aliye kusudiwa na uchawi huu, kama
hana kinga, ata andamwa na mikosi mikubwa na mizito katika
maisha yake yote.
JINSI YA KUJIKINGA DHIDI YA UCHAWI HUU
Kujikinga
na uchawi huu inabidi ufanyiwe zindiko ama upate kinga maalumu
ya kuficha kivuli chako. Hii itawafanya wachawi washindwe
kukuona katika rada zao za kichawi, na wachawi huwa hawawezi
kumloga mtu ambae haonekani katika rada zao, kwa sababu
wanawakuwa hawajui nguvu zake ziko wapi wala silaha zao
haziwezi kumshambulia mtu ambae haonekani kwenye rada zao.
Ukiwa
na kinga hii, hakuna uchawi wa aina yoyote ile unao weza
kufanyika juu yako, iwe ni uchawi wa kukusababishia madhara, au
uchawi wa mahaba kukufunga kimapenzi.
JINSI YA KUFICHA KIVULI CHAKO KISIONEKANE NA WACHAWI
Kuficha kivuli chako kisonekane na wachawi, fanya kama ifuatavyo
i. Chukua nywele za saluni
ii. Chukua mzizi wa mti ulio katisha njia
iii.
Chukua tawi la mti unaitwa Ututukanga. Huu mti wa Ututukanga
unapatikana porini na baharini na huwa linaonekana shina lake na
matawi yake tu, lakini mzizi wake huwa hauonekani.
iv. Unachukua mti unaitwa Msonihya
v. Unasaga pamoja na mti unaitwa mwavi.
vi.
Baada ya hapo unachukua kuku mweusi, unamfunga kwenye kitambaa
cheusi bila kumchinja, unachukua chungu cheusi, unamuunguza mpaka
anakuwa mkaa, halafu unamsaga pamoja na miti iliyo tajwa hapo
juu, unachanganya na mafuta ya simba.
vii. Unachukua buja ama dulya la ugali wa kilioni
viii.Unachukua
kamba ya kitanda alicho lalia maiti, au kama maiti ipo kwenye
nyumba ya nyasi, unachomoa nyasi wakati maiti imo ndani.
ix. Unachimba mzizi wa mti unaitwa mputika bila kivuli chako kugusa mti..
x. Unaunguza vyote kwa pamoja ukiwa na kaniki nyeusi bila kuvaa nguo yoyote usiku wa manane
xi. Unaipika njia panda pamoja na mafuta ya usiku.
Baada ya hapo, mtu atachanjiwa au kujichanja mwenyewe na kuoga au kuogeshwa dawa hiyo.
Basi wachawi watakuwa wakijaribu kutaka kukutupia uchawi, wanakuwa hawakauoni kwenye rada zao za kichawi.