test

Jumamosi, 17 Desemba 2016

WAZIRI MKUU AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA, AWATAKA WASIOENDELEZA MASHAMBA ARUMERU KUNYANG’ANYWA




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia burudani ya wanawake wa kimasai baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa eneo la Kwamrombo wilayani Arusha ambao walijipanga kwa wingi barabarani na kumshawishi kusimama ili kuzungumza nao. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 27, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kizungumza na wananchi wa kijiji cha Ormapinu wilayani Arusha ambao wlijipanga kwa wingi barabarani na kumshawishi kusismama ili kuwasikiliza. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 27, 2016.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali itawanyang’anya ardhi wamiliki wote wa mashamba makubwa wilayani Arumeru ambao hawajayaendeleza kwa sababu wamekiuka mkataba wa umiliki.

Amesema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi atakuja mkoani Arusha kwa ajili ya kufanya mapitio ya mashamba yote makubwa ambayo hayajaendelezwa na kuyarudishwa Serikalini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Desemba 17, 2016) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Arumeru na wananchi wa kijiji Bwawani na kitongoji cha Mapinu katika kata ya Nduruma akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Arusha.

“Tufanya mapitio ya kila shamba ili kujua linamilikiwa na nani na alipewa lini na tangu alipokabidhiwa amefanya nini. Shamba lisiloendelezwa litarudisha kwa wananchi. Kama mtu ameshindwa kupata mtaji kwa muda wa miaka 10 atapata leo,” amesema.

Amesema Serikali haiko tayari kuona wananchi wakinyanyaswa kwa kukosa ardhi ya kilimo kwa sababu ya watu wachache kumiliki maeneo makubwa bila ya kuyaendeleza..

"Ninataarifa kwamba hapa Arumeru kuna baadhi ya wawekezaji wanamiliki mashamba makubwa na hawajayaendeleza. Wengine wanakodisha kwa wananchi ili kujipatia fedha kinyume na mikataba yao ya umiliki. Hatutawavumilia,” amesema.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI ZAIDI

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx