WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango amesema vijana ndiyo wanaweza kuleta mapinduzi ya sekta ya viwanda vinavyojengwa.
Dk.Mpango
ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Maonesho ya Viwanda
yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, ameseama
vijana lazima wachangamkie fursa ya viwanda pamoja na ujasiriamali.
Amesema
nafasi za ajira ni chache ikilinganishwa na idadi ya vijana wanaohitaji
hivyo sekta binafsi ndiyo inaajiri sehemu kubwa ikiwemo kujiajiri. Dk. Mpango amesema sekta ya viwanda inahitaji rasimali watu ambao ni vijana wa kufanya hivyo kwa ujuzi wao.
Aidha
amesema kila mtu anatakiwakulipa kodi ili serikali iweze kutoa huduma
kwa wananchi na kodi isipotumika kwa malengo wananchi wanaweza kuhoji
kodi i yao.
Dk.
Mpango amesema serikali haitaki kuibana sekta binafsi ishindwe kupumua
kutokana na kodi kinachofanyika kuangalia uwezo wa ulipaji kodi kwa
kilakinachozalishwa. Waziri huyo ametoa maagizo kwa Mamlaka ya Chakula Dawa (TFDA), kuwatembelea wajasiriamali ili kuweza kupata changamoto zao.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi habari
mara baada ya kutembelea maonesho ya viwanda yanayoendelea katika
viwanja vya sabasaba leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji
wa Global Education Link (GEL),Abdulmalik Mollel wakati alipotembelea
banda hilo katika viwanja vya sabasaba leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akitoa maagizo kwa Meneja
Uhusiano kwa Umma wa TFDA, Gaudensia Simwanza wakati alipotembelea banda
la TFDA katika viwanja vya sabasaba leo jijini Dar es Salaam.
Wananchi
wakipata huduma katika banda la majani ya chai katika maonesho ya
viwanda yanayoenelea katika viwanja sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wananchi
wakipata huduma katika banda la Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji
katika maonesho ya viwanda yanayoenelea katika viwanja sabasaba jijini
Dar es Salaam