Vijana wametakiwa kubeba uchumi wa viwanda wa Tanzania inayojengwa katika serikali ya awamu ya Tano ya Dk. John Pombe Magufuli.
Hayo
ameyasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka wakati wa
semina ya vijana iliyofanyika katika maonesho ya viwanda yanayoendelea
katika viwanja vya Sabasaba leo jijini Dar es Salaam.Amesema semina
imefika muda mwafaka kutokana na nchi kwenda katika sekta ya viwanda
ambapo vijana ndio sehemu yao.
Amesema
sekta ya viwanda inategemea vijana ambao ndio waendeshaji wa viwanda
katokana na ujuzi wao wa kuendea viwanda hivyo.Nae Mwakilishi wa Taasisi
ya Doris Mollel Foundation, amesema vijana wanatakiwa kutumia fursa ya
viwanda pamoja na ujasirimali na kuachana na kufikiria suala la
kuajiriwa.
Amesema
Taasisi Doris Mollel Foundation,imeona inawajibu wa kutoa elimu kwa
vijana katika kuendea sekta ya viwanda.Amesema kuwa kila mmoja akatumia
nafasi yake vizuri Tanzania inaweza kuondoka ilipo sasa na kusogea
sehemu nyingine katika uchumi wa viwanda .
Akifunga
simina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link
(GEL),Abdulmalik Mollel amesema hakuna tatizo la ajira kwa vijana
kuajiriwa kinachofanya vijana na kukosa mafunzo ya kazi ambayo
wanakwenda kufanya.Amesema kutokana na mafunzo hayo kupitia maonesho ya
viwanda atafanya mafunzo vijana ambao wanakwenda kutumika katika viwanda
wakiwa wanakitu kichwani.
Mollel
amesema hakuna mtu anaweza akamuachia kijana kiwanda kwa elimu
alioipata anatachotaka mwajiri ni kijana mwenye ujuzi wa kutumikia
kiwanda chake.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka akizungumza katika
ufunguzi wa semina ya vijana kuelekea uchumi wa viwanda iliyofanyika
katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Taasisi Doris Mollel Foundation, Erick Kajwahura akizungumza katika
semina vijana kuelekea uchumi wa viwanda iliyofanyika katika viwanja vya
Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa I-Learn East Afrika Limited, Noelah Ntukamazina akizungumza
katika semina kuelekea uchumi wa viwanda iiyofanyika katika viwanja vya
sabasaba jijini Dar es Salaam leo
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Education Link (GEL),Abdulmalik Mollel akifunga
semina ya kuelekea uchumi wa viwanda iiyofanyika katika viwanja vya
sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu
vijana wakiwa semina ya kuelekea uchumi wa viwanda iiyofanyika katika
viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.picha na Emmanuel
Massaka,Globu ya jamii.