Leo Desemba 9 Tanzania Bara imeazimisha miaka 55 tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa wakoloni mwaka 1961.
Maadhimisho hayo yamepambwa na shughuli mbalimbali za kijeshi lakini pia ngoma za asili kutoka kwa makundi mbalimbali.
Mbali
na mambo hayo yaliyoonekana kuwavutia wengi, jambo lingine
lililowafurahisha ni pale Rais Dk Magufuli alipoamua kutembea
kiukakamavu kama mwanajeshi mara baada ya kumaliza kukagua gwaride
katika maadhimisho haya ya 55 ya uhuru.
Hapa chini ni video ra Rais Dk Magufuli akitembea kiukakamavu baada ya kukagua gwaride katika sherehe za uhuru.