*Wamo pia wa sekta viwanda, kilimo
BAADA ya kusitisha ajira za umma kwa takribani miezi tisa,
Serikali imesema katika mwaka huu wa bajeti itaajiri watu 71,496
Hata
hivyo, licha ya kutaja idadi ya watumishi wapya wanaotarajiwa kuajiriwa
katika mwaka huu wa fedha, Serikali haijaweka bayana ni lini hasa ajira
hizo zitaanza kutolewa licha ya kuwa imebaki miezi sita mwaka wa bajeti
kumalizika.
Akijibu
maswali yaliyoulizwa juu ya lini Serikali itaanza kutoa ajira, baada
ya kuzisitisha kwa muda, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais
(Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Florence Temba, alisema Serikali
inatoa fursa za ajira kama ilivyoelezwa katika mpango mwaka wa fedha
2016/17.
Katika
majibu hayo aliyoyatoa kwa niaba ya Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean
Ndumbaro, yalibainisha kwamba ajira hizo zitakuwa kwenye sekta ya elimu,
afya, kilimo na mifugo.