Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam,Paul Makonda akizungumza nawafanyabiashara ndogo ndogo marufu
kama Machinga mtaa wa Kongo na kusikiliza kero zao leo jijini Dar es
Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam,Paul Makonda akizungumza wafanyabiashara wa soko kuu la Kariakoo
nakusikiliza kero zao leo jijiji Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa na viongozi mbalimbli akikagua soko la Kariakoo.
Ofisa Tawala wa wilaya
ya Ilala, Edward Mpogolo akifafanua jambo katika mkutano
wawafanyabiashara ndogo ndogo Machinga mtaa wa Kongo leo jijiji Dar es
Salaam.
Wafanyabiashara na wananchi wakimsikiliza mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda
WAFANYABIASHARA ndogo
ndogo wa Kariakoo wametakiwa kuuza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya
ndani ili kukuza uchumi wa viwanda. Hayo ameyasema leo na Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokutana na wafanyabiashara wandogo
wandogo wa Kariakoo, amesema bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vya
ndani zikipata soko nchi itapata mapato pamoja na kukuza uchumi wa nchi
yetu.
Amesema serikali iko
pamoja na wamachinga kuhakikisha wanafanya biashara kwa mujibu wa sheria
kwa kuuza vitu vyenye ubora na wakibaini kuwepo kwa vitu ambavyo
vinahatarisha maisha ya watanzania watachukuliwa hatua mara moja.
Makonda amesema ni
marufuku wageni kutoka nje ya nchi kufanyabiashara ya umachinga katika
jiji la Dar es Salaam wao wanatakiwa kuleta utaalam tu. Aidha amewaasa
wamachinga kuwafichua wale ambao wanaweka rebo katika bidhaa wakati
hawazalishi wenyewe.
Makonda amesema katika maeneo ambayo wanafanyia kazi wamachinga kufuata sheria na kanuni zilizowekwa bila kuharibu utaratibu.