Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole
amesema atahakikisha chama hicho kinakuwa ni cha wanyonge na kuendelea
kuwa kimbilio la wasio na sauti.
Polepole
ametoa kauli hiyo leo wakati akikabidhiwa rasmi ofisi na Katibu
anayemaliza muda wake Nape Nnauye katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya
chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.
Polepole
alisema kwa misingi ya chama hicho imejengwa kuwasaidia na kuwa tete
wanyongo hivyo katika muda wake wa uongozi atahakikisha chama kinasimama
katima misingi hiyo ya kuanzishwa kwake.
“Msingi wa chama chetu ni utetezi wa wanyonge, tutahakikisha kinaendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti,” alisema Polepole.
Aidha,
katibu huyo alisema kuwa katika kutekeleza majukumu yake aliyokabidhiwa
leo na mtangulizi wake, atahakikisha anajikita zaidi katika kazi za
itikadi zaidi kuliko uenezi kwa kuwa itikadi ndiyo inayokibeba chama.
Polepole
alitumia muda huo kumshukuru Nape Nnauye anayemaliza muda wake na
kusema kuwa ni kiongozi imara na kuwa katika muda wake aliweza
kuitumikia vyema nafasi yake. Lakini pia alisema japo anamaliza muda
wake, lakini atakuwa akimuhitaji mara kwa mara kwa ajili ya ushauri na
mambo mengine.
Wakati
huo huo, Polepole amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
na Halmashauri Kuu ku kumwamini na kumpa majukumu hayo makuwa.