Mkoa
wa Dar es Salaam utaanza kutoa huduma za kisheria kwa wananchi wote
bure kupitia wanasheria 35 ambao wamegawanywa katika wilaya zote za mkoa
huo, kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi
wake.
Makonda
amesema hatua hiyo itasaidia kutatua kero za wananchi ambao wamekuwa na
uelewa mdogo wa sheria na kusababisha wananchi hao kukosa haki zao
hususani katika masuala ya ardhi,mirathi, malalamiko ya rushwa na
kufukuzwa kazi na waajili wao kinyume na sheria.
“Hawa
vijana tulionao ni vichwa wanaenda kututatulia kero wananchi wa Dar es
Salaam, tunawakabidhi leo kwa wakuu wa wilaya tena kwa wilaya zote tano
na watapangiwa majukumu yao na niwataarifu tu wananchi kuanzia mwakani
mwezi wa kwanza nenda kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya utawakuta
wanasheria kabla hujachukua hatua yeyote ya kwenda mahali mahakamani
hakikisha unapitia wanasheria wetu hawa ukiona kama
unadhulumiwa.Watakupa msingi wa kisheria na hautalipa hata senti tano,”
alisema Makonda.
Makonda
alisema ili kutatua changamoto hizo kila Wilaya itakuwa na mawakili,
Kinondoni (9), Temeke (4), Ubungo (6), Kigamboni (6) na Ilala (6).