Hii
ni ajali nyingine ya Sugu aliyoipata Januari 10, 2015 kwenye mlima wa
Kitonga baada ya gari lake breki kufeli na hakuna mtu yeyote
aliyejeruhiwa
MBEYA: Taarifa zilizoripotiwa na kituo cha runinga cha ITV leo Desemba
17, 2016 zinasema kuwa Mbunge wa Jimbo loa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph
Mbilinyi amenusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea eneo la
Iyunga jijini Mbeya baada ya gari lake kufeli break na kumgonga mtoto
’15’ ambaye amefariki wakati akipelekwa hospitali.
Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa askari polisi wanne wamejeruhiwa baada
ya kupata ajali wakati wakielekea kwenye ajali hiyo aliyopata mbunge
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’
Pia imeelezwa kuwa, Mbunge Sugu ametoka akiwa salama huku dereva wake
aliyekuwa akiendesha gari hilo, Gabriel Andrew (43) anashikiliwa na
Jeshi la Polisi mkoani humo.