Viongozi wa Ukawa, Edward Lowassa wa Chadema na Maalim Seif Sharif
Hamad wa CUF wamekwenda kumjulia hali Mwenyekiti wa NCCR–Mageuzi, James
Mbatia baada ya kutoka kwenye matibabu nchini India, ambako alifanyiwa
upasuaji wa mguu.
Mbatia,
ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, alifanyiwa upasuaji huo Novemba 14
katika Hospitali ya Zydus Ahmedabad Gujarat baada ya mguu huo kumsumbua
kwa takribani miaka 37.
Akiwa
nyumbani kwa Mbatia Mbezi Beach, Lowassa amesema, “Nimekuja kumuona
mheshimiwa (Mbatia). Nimefurahi zaidi baada ya kunieleza anaendelea
vizuri. Watanzania waendelee kumuombea na siku zijazo atazidi kupata
nafuu zaidi.”Maalim Seif alimpa pole na kusema, “Binadamu ndivyo tulivyoumbwa, kuna kuumwa na usipoumwa tushukuru Mungu.”
Akizungumzia
matibabu yake, Mbatia alisema ilitumika teknolojia ya kisasa kwenye
upasuaji huo uliochukua saa nne kutokana na tatizo la mguu lililoanza
akiwa na umri wa miaka 15.