Kaimu Kamishna Jenerali
wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) akipokea vifaa vya
michezo kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SAN LAM Life
Insurance, Bw. Samuel Mika(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Fedha na
Utawala wa Jeshi hilo, Kamishna Gaston Sanga(wa kwanza kushoto) ni Afisa
Uhusiano wa Kampuni ya SAN LAM, Bw. Rishia Kileo. Vifaa hivyo
vitatumiwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza katika Mashindano
ya Kijeshi yanayotarajiwa kufanyika Zanzibar mwezi huu Desemba, 2016.
Kaimu Kamishna Jenerali
wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akitoa neno la shukrani kwenye
hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na Kampuni
ya SAN LAM Life Insurance. Hafla hiyo imefanyika leo Desemba 06, 2016
katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Kamishna wa
Magereza Gaston Sanga(kulia) ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni SAN LAM
Life Insurance, Bw. Samuel Mika.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya SAN LAM Life Insurance, Bw. Samuel Mika akitoa maelezo mafupi
kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Jeshi la Magereza leo Desemba
06, 2016 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar
es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Michezo ya Jeshi la Magereza, SACP. Gideon Nkana akitoa utambulisho
mfupi katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Jeshi la Magereza
leo Desemba 06, 2016 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna Jenerali
wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati walioketi) akiwa katika
picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na
Wawakilikilishi wa Kampuni ya SAN LAM Life Insurance(waliosimama). hafla
hiyo ya makabidhiano ya vifaa vya michezo imefanyika leo Desemba 06,
2016 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es
Salaam.