MADEREVA
wa bodaboda wametajwa kuongoza kufanya matukio ya ukatili wa kijinsia
mkoani Pwani yanayohusisha ubakaji, ulawiti na kuwapa mimba wanafunzi.Imeelezwa
kuwa, kati ya watuhumiwa 10 wa makosa hayo ya ukatili, watatu ni
madereva wa bodaboda.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi, alisema hayo alipokuwa akizungumza na madereva wa bodaboda na wananchi na kusema kuwa hilo ni janga ambalo linapaswa kupigiwa kelele na jamii yote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi, alisema hayo alipokuwa akizungumza na madereva wa bodaboda na wananchi na kusema kuwa hilo ni janga ambalo linapaswa kupigiwa kelele na jamii yote.
Alisema
matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Pwani yameongezeka kutoka 257 kwa
kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka jana na kufikia 310 kipindi
kama hicho mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la makosa 53.
Aidha
imebainika kuwa madereva wa bodaboda wanaongoza kwa kufanya matukio
hayo ya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na ubakaji, ulawiti, kuwapa
mimba wanafunzi.
Kamanda
Mushongi alisema utafiti uliofanywa na dawati la jinsia na watoto
mkoani hapo, limebaini kwamba baadhi ya madereva bodaboda hujihusisha na
vitendo hivyo jambo ambalo linapaswa kupigwa vita.“Madereva hao
wasaidiane kuwafichua wale ambao wamekuwa wakiitia doa kazi hiyo na
kuwachafua mbele ya uso wa jamii na kuanzisha timu za ulinzi na usalama
ili kupeana elimu na kutoa taarifa juu ya vitendo vya ukatili wa
kijinsia,” alisema.
Alisema
kupitia umoja wao wapinge matendo yote ya ukatili na udhalilishaji na
kuwalinda watoto ili kupambana dhidi ya vitendo vya ukatili kwa lengo la
kupunguza na kutokomeza vitendo hivyo.
Hata
hivyo, Mushongi aliwaomba wazazi kuhakikisha wanasimamia malezi ya
watoto kwa karibu, badala ya kuwaachia kina mama pekee ambao baadhi yao
huwaachia wasichana wa kazi jukumu hilo.
Alibainisha
suala hilo la wazazi kuwa mbali husababisha baadhi ya watoto
kujitumbukiza katika vitendo vya ngono wakiwa katika umri mdogo na
kusababisha kupata ujauzito, ama kuambukizwa magonjwa ikiwemo virusi vya
Ukimwi.
Via>>Habarileo