Mabalozi hao wamesema hatua hiyo ya itasaidia kukuza shughuli za utalii na pato la taifa kwa ujumla.
Balozi wa Brazil nchini, Carlos Alfonso Puente na Balozi wa Kenya, Chirau Makwere wametoa pongezi hizo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es salaama jana.
Taarifa kutoka ofisi ya makamu wa Rais, ilisema Balozi Puente alisema kutokana na nchi hiyo kuwa ni miongoni mwa nchi kadhaa duniani zenye viwanda wa kutengeneza ndege, serikali ya Tanzania ina nafasi nzuri ya kununua ndege nchini Brazil hasa kulingana na mahusiano mazuri na ya muda mrefu yaliyopo kati ya nchi hizo mbili.
Aidha, Samia alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wa nchini Brazil kuja nchini kutangaza bidhaa wanazotengeneza hasa ndege kama hatua ya kuimarisha uhusiano wa biashara kati nchi hizo mbili.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais katika mazungumzo yake na Balozi wa Kenya alisisitiza kudumishwa na kuendelezwa kwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Kenya hasa katika uimarishaji wa biashara na uwekezaji.
Pia alitoa wito maalum kwa Watanzania kuchangamkia fursa ya kufanya biashara na nchi ya Kenya kutokana na nchi mbili kuwa na mahusiano mazuri ya kibiashara.