Skip to content
Uongozi wa Klabu ya Yanga kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake, Clement
Sanga amemtambulisha George Lwandamina kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo
katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Yanga, Jwangwani jijini Dar es
Salaam.
Katika hafla hiyo aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm amepewa cheo cha Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo.
Lwandamina ni raia wa Zambia ambaye alikuwa mchezaji na kocha wa timu ya
taifa ya Zambia kabla ya kuikacha timu hiyo na kujiunga na Yanga ya Dar
es Salaam, Tanzania.
Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
xxxxxxxxxxxxx